Diplo Internet Governance Community

Stay networked. Get informed. Broadcast your projects.

HAKI NA KANUNI 10 ZA MTANDAO WA INTERNET

HAKI NA KANUNI 10 ZA MTANDAO WA INTERNET

Hati hii inafafanua haki na kanuni kumi muhimu ambazo ni msingi kwa uongozi bora wa Mtandao wa Internet (Mtandao). Zimekusanywa na Muungano wa Haki na Kanuni za Mtandao (Dynamic Coalition on Internet Rights and  Principles), ambao ni mkusanyiko wazi wa watu binafsi na mashirika yanayozingatia haki za kibinadamu katika Mtandao. Kanuni hizi zinazingatia viwango vya haki za kibinadamu vya kimataifa na zimetokana na Mkataba wa Haki na Kanuni za Mtandao ambao unatengenezwa na muungano huu.
WWW.INTERNETRIGHTSANDPRINCIPLES.ORG

 

Mtandao umetoa fursa ya kipekee ya utambuzi wa haki za kibinadamu. Pia jukumu lake katika maisha yetu ya siku
kwa siku linaendelea kuongezeka. Hivyo, ni muhimu kwa wahusika wote, umma na binafsi, kuheshimu na kulinda haki za kibinadamu kwenye Mtandao. Hatua pia lazima zichukuliwe ili kuhakikisha kwamba vile ambavyo Mtandao unatumika na kuzidi kukua, haki za kibinadamu zinatekelezwa kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo. Kwa minajili ya kuafikia maono haya ya Mtandao ambapo haki za kibinadamu zinatimizwa, haki na kanuni 10 za Mtandao ni:

1) Kupatikana Kote na Usawa Binadamu wote wamezaliwa huru na sawa kwa hadhi na haki ambazo lazima ziheshimiwe, zilindwe na kutimizwa kwa mazingira ya Mtandao.

2) Haki na Uadilifu kwa Jamii Mtandao ni fursa ya kukuza, kulinda na kutekeleza haki za kibinadamu na maendeleo ya uadilifu katika jamii. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu haki za binadamu wengine wote katika mazingira ya
Mtandao.

3) Upatikanaji Kila mtu ana haki sawa ya kupata na kutumia Mtandao salama na wazi.

4) Kujieleza na Kujiunga Kila mtu ana haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari kwa uhuru kwenye Mtandao bila udhibiti au kuingiliwa. Kila mtu pia ana haki ya kujiunga kwa hiari kupitia na kwenye Mtandao, kwa madhumuni ya kijamii, kisiasa, kitamaduni au sababu nyingine.

5) Faragha na Ulinzi wa Takwimu Kila mtu ana haki ya faragha akiwa Mtandaoni. Hii inajumuisha uhuru wa kutofuatiliwa, haki ya kutumia msimbo (encryption), na haki ya kutokujitambulisha Mtamboni. Kila mtu pia ana
haki ya ulinzi wa takwimu, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa ukusanyaji wa takwimu binafsi, uhifadhi, usindikaji, uondoaji na utoaji taarifa.

6) Maisha, Uhuru na Usalama Haki za maisha, uhuru, na usalama lazima ziheshimiwe, zilindwe na zitimizwe Mtandaoni. Haki hizi lazima zisikiukwe,au kutumiwa kukiuka haki zingine katika mazingira ya Mtandao.

7) Utofauti Utamaduni na lugha mbalimbali kwenye Mtandao lazima kukuzwa, na ufundi na ubunifu wa sera lazima zitiliwe maanani ili kuwezesha uwepo wa wingi wa kujieleza.

8) Usawa wa Mitandao Kila mtu ana haki ya kufungua kupata maudhui ya Mtandao kote, bila ubaguzi kipaumbele, kuchujwa au kudhibiti trafiki kwa misingi ya kibiashara, kisiasa au mengine.

9) Viwango na Taratibu Usanifu wa Mtandao, mifumo ya mawasiliano, hati na jinsi za takwimu katika Mtandao zitatengenezwa kwa viwango vya wazi ili kuhakikisha utangamano kamili, ushirikishaji na fursa sawa kwa wote.

10) Uongozi Bora Haki za kibinadamu na uadilifu wa kijamii lazima ziwe kwenye misingi ya utawala na sheria za utumizi na uongozi wa Mtandao. Hii itakuwa kwa njia ya uwazi, ushirikishaji wa mataifa, ujumuishaji na
uwajibikaji.

Views: 216

Comment

You need to be a member of Diplo Internet Governance Community to add comments!

Join Diplo Internet Governance Community

Members

Groups

Follow us

Website and downloads

Visit Diplo's IG website, www.diplomacy.edu/ig for info on programmes, events, and resources.

The full text of the book An Introduction to Internet Governance (6th edition) is available here. The translated versions in Serbian/BCS, French, Spanish, Arabic, Russian, Chinese, and Portuguese are also available for download.

Interviews


Karlene Francis (Jamaica)
Ivar Hartmann
(Brazil)
Elona Taka (Albania)
Fahd Batayneh (Jordan)
Edward Muthiga (Kenya)
Nnenna Nwakanma (Côte d'Ivoire)
Xu Jing (China)
Gao Mosweu (Botswana)
Jamil Goheer (Pakistan)
Virginia (Ginger) Paque (Venezuela)
Tim Davies (UK)
Charity Gamboa-Embley (Philippines)
Rafik Dammak (Tunisia)
Jean-Yves Gatete (Burundi)
Guilherme Almeida (Brazil)
Magaly Pazello (Brazil)
Sergio Alves Júnior (Brazil)
Adela Danciu (Romania)
Simona Popa (Romania)
Marina Sokolova (Belarus)
Andreana Stankova (Bulgaria)
Vedran Djordjevic (Canada)
Maria Morozova (Ukraine)
David Kavanagh (Ireland)
Nino Gobronidze (Georgia)
Sorina Teleanu (Romania)
Cosmin Neagu (Romania)
Maja Rakovic (Serbia)
Elma Demir (Bosnia and Herzegovina)
Tatiana Chirev (Moldova)
Maja Lubarda (Slovenia)
Babatope Soremi (Nigeria)
Marilia Maciel (Brazil)
Raquel Gatto (Brazil)
Andrés Piazza (Argentina)
Nevena Ruzic (Serbia)
Deirdre Williams (St. Lucia)
Maureen Hilyard (Cook Islands)
Monica Abalo (Argentina)
Emmanuel Edet (Nigeria)
Mwende Njiraini (Kenya)
Marsha Guthrie (Jamaica)
Kassim M. AL-Hassani (Iraq)
Marília Maciel (Brazil)
Alfonso Avila (Mexico)
Pascal Bekono (Cameroon)

© 2021   Created by Community Owner.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service